KARIBU SANA

Sunday, December 14, 2008

TENGA NA MALINZI, MMOJA KUANGUA KILIO LEO


Kuanzia leo asubuhi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekuwa na uchaguzi mkuu wa nafasi mbalimbali ambapo kabla ya yote aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo, Leodgar Tenga (pichani juu) akitangaza kujitoa katika nafasi hiyo baada ya muda wake kumalizika ingawa bado anagombea tena nafasi hiyo akichuana vikali na akiyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jamal Malinzi. Baadaye Leodgar Tenga alikwenda kuomba tena kura za kumpa nafasi ya kuongoza TFF kwa miaka minne ijayo.
Brother Jamal Malinzi, ambaye anagombea nafasi ya Urais wa TFF na Leodgar Tenga, akiwa kama amelowana wakati wajumbe wa mkutano mkuu wakiendelea kupiga kura katika uchaguzi huo unaondelea katika Jengo la NSSF Water Front jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment