Hata hivyo, Nakaaya aliye dada wa Miss World Africa 2005-06, Nancy Sumari alikiri kwamba yupo kwenye penzi zito na Dead Prez ambaye hupiga bao zaidi kupitia mashairi yenye ujumbe wa Kisiasa.
“Sijafunga ndoa mimi ila Dead Prez ni mpenzi wangu na muda utakapokuwa tayari nitawaambia Watanzania. Sina haja ya kufanya siri,” alisema Nakaaya.
‘Mdada’ huyo alitoa kauli hiyo, akijibu swali la mwandishi wetu ambaye alimuuliza kuhusu madai kwamba amefunga ndoa ya siri na Dead Prez.
Awali, gazeti hili lilipokea udaku kutoka kwenye chanzo chake ambacho ni ndugu na Nakaaya, ulioweka wazi kuwa mwanamuziki huyo amefunga ndoa ya siri visiwani Zanzibar.
Chanzo hicho kilidai kwamba Nakaaya na Dead Prez waliamua kuoana kwa siri ili kukwepa ‘matochi’ ya waandishi wa habari.
“Huu ndiyo ukweli, Nakaaya ameolewa na Dead Prez wiki iliyopita, amefunga ndoa ya siri,” tulikinukuu chanzo chetu.
Pamoja na ‘data’ hizo kutoka kwa chanzo chetu, Nakaaya aliendelea kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kuchukua maneno ya mtu mwingine kwa kuwa yeye ndiye mhusika, kwahiyo kauli yake ndiyo ichukuliwe.
Nakaaya ambaye alianza kung’ara kupitia shindano la Project Fame 2007, alisema: “Kuna sababu gani ya kuficha ukweli? Na sina haja ya kufunga ndoa ya siri, kwahiyo hata mahari bado, achilia mbali kufunga ndoa, mambo yakiwa tayari nitasema.”
Licha ya kukanusha madai hayo, baadhi ya watu wa karibu na ‘modo’ huyo waliendelea kusisitiza kuwa ni kweli Nakaaya amefunga ndoa ya siri na Dead Prez.
“Sisi tumesema amefunga ndoa ya siri, inamaana kuna vitu anaficha, kwahiyo waandishi mnapomuuliza ni lazima akatae, lakini ukweli ni huu, amefunga ndoa ya siri bila watu kujua, hata mdogo wake Nancy hafahamu kama dada yake ameolewa,” alisema mmoja wa watu wa karibu na Nakaaya kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Nakaaya na Dead Prez wamekuwa wakidaiwa kula ‘urojo’ tangu walipoimba pamoja wimbo Mr. Politician remix. Inaelezwa kuwa dada yetu ameangukia kwenye penzi la Mmarekani huyo baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Ibaragi Heiji.

No comments:
Post a Comment