KARIBU SANA

Monday, April 6, 2009

Tuzo za muziki Tanzania 2008/2009

Tuzo za Muziki za Tanzania, zimekwishatolewa usiku wa kuamkia jana, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na wasanii mbalimbali wameweza kuibuka na ushindi katika vipengele (category) kadhaa. Hata hivyo, kila mwaka mara baada ya wasanii kupewa tuzo, kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale kutoka kwa wadau wa muziki nchini wakidai kuwepo kwa aina ya ubabaishaji katika utolewaji wa tuzo hizo. Je, kwa upande wako wewe mdau wa mtandao huu namba moja wa burudani Tanzania, una maoni gani katika tuzo za mwaka huu? Na unafikiri nini kingefanyika au kifanyike mwakani? Toa maoni yako sasa, lengo likiwa ni kuwekana sawa katika sanaa ya Tanzania.
Kama kawa, Kamati ya Tuzo za Muziki Tanzania, imerudia kasoro za upangaji wa vipengele vya muziki na wasanii walioteuliwa kuwania ‘awadi’ hizo kwa msimu wa mwaka 2008/09
Kundi la Blue 3 kutoka nchini Uganda, katika tamasha hilo walitoa bonge la shoo.

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Nameless (kushoto) naye aliibuka na tuzo ya msanii Bora Afrika Mashariki, akipigwa busu na Hoyce Temu.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Khaleed Mohamed 'TID' naye alikuwa mmoja wa wasindikizaji kama anavyoonekana pichani akimshika mkono Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Idd Azzan
Mkali wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yessaya, naye alipanda jukwaani kufanya makamuzi ya nguvu.

No comments:

Post a Comment