
Rais Kikwete amefanya uteuzi huo Februari 9, mwaka huu ambapo uteuzi huo ulienda sambamba na kumpandisha cheo mkuu huyo mpya kuwa Meja Jenerali kutoka cheo cha Brigedia Jenerali.
Kitundu, alivishwa cheo hicho na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwanyange kwa niaba ya Rais Kikwete katika hafla fupi iliyofanyika Kambi ya JKT Mgulani, ambayo ilihudhuriwa na maafisa, askari na watumishi wa umma kutoka vikosi vya JKT mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Pichani: Meja Jenerali Kitundu akiongea na maafisa, askari na watumishi wa JKT mara baada ya kupewa wadhifa huo
No comments:
Post a Comment