KARIBU SANA

Saturday, February 28, 2009

NANI ZAIDI KATI YA JOHARI NA NORA?

Baada ya kinyang’anyiro kikali kati ya Bendi mbili za muziki wa dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na Akudo Impact ‘Chuo cha Masauti’ kumalizika ambapo matokeo tutawaletea baadaye, wiki hii Mtandao wako wa burudani nchini, unakuletea shindano lingine kali zaidi la wasanii wa kike katika anga za filamu nchini, nao si wengine bali ni Blandina Chagula ‘Johari’ na Nuru Nassor ‘Nora’. Hawa wote walianza kuonekana kwenye michezo ya kuigiza runingani, kupitia kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar es Salaam. Walisonga mbele na kuonesha umahiri wao kwa kushiriki filamu mbalimbali za hapa nchini. Kwa upande wake, Nora ameshashiriki filamu za Sikitiko Langu, Sweet Backreena, Upande wa Pili wa Ndoa, Johari na nyingine nyingi. Johari yeye ameshakamua kwenye Johari, Yellow Banana, Wicked Love, Fake Pastors, From China With Love, My Wife na nyingine kibao.
Kazi kwako msomaji wa mtandao huu, Nani Zaidi?

1 comment:

  1. mambo nora na johari mimi niko america ninamyaka kuminatatu niriona mikandamurijeza irinifuraisha sana nikama sikitiko langu oke ukitaka my email is aristideelias@ymail.com oke syou

    ReplyDelete