KARIBU SANA

Wednesday, February 25, 2009

ONESHO KUBWA LA MAVAZI LAJA

Mbunifu wa mavazi wa muda mrefu, Fatuma Amour, anatarajia kufanya onesho la mavazi Machi 07, mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live (zamani Malaika) uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo itakuwa ni siku ya wanawake duniani.
Katika onesho hilo Fatuma amesema kutakuwa na mitindo mbalimbali ya mavazi kama vile ya Kitanzania, Kirasta, Kimasai na mingineyo.

Pichani muandaaji wa shughuli hiyo, Fatuma Amour, akielezea mambo yatakayojiri siku hiyo.



Baadhi ya vimwana watakaoshiriki onesho hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment