KARIBU SANA

Sunday, November 30, 2008

KIKWETE APANGUA MAKATIBU WAKUU, MGONJA ANG'OKA WIZARA YA FEDHA

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya makatibu wakuu na naibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

Katika mabadiliko hayo yaliyogusa wizara 13, wameteuliwa makatibu wakuu wapya wanne na manaibu watatu, huku akihamisha makatibu wakuu wanane na naibu mmoja.

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, imetaja baadhi ya sababu za mabadiliko hayo kuwa ni pamoja na baadhi ya watendaji hao kustaafu kwa mujibu wa sheria kati ya Agosti na Novemba mwaka huu.

Wizara ambazo zimeguswa na mabadiliko hayo ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na nyingine tisa.

Aidha, katika uteuzi huo unaoanza mara moja, Rais Kikwete amewateua wasaidizi wake wawili wa Ikulu kuwa naibu makatibu wakuu.

Walioteuliwa kuwa makatibu wakuu ni Alhaj Ramadhan Kijja anayekwenda Wizara ya Fedha na Uchumi kushika nafasi inayoachwa wazi na Gray Mgonja aliyeelewa kuwa katika likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Wengine ni Dk Florens Turuka anayekwenda Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Joyce Mapunjo kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara na Andrew Nyumayo anayekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Alhaj Ramadhan Kijja aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi amepandishwa cheo kuziba nafasi ya bosi wake. Dk Turuka alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mapunjo alikuwa na wadhifa huo, Wizara ya Miundombinu na Nyumayo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Makatibu wakuu waliohamishwa Wizara ya ni pamoja na Paniel Lyimo aliyekuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko sasa amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Ladislaus Komba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana na nafasi yake kuzibwa na Kijakazi Mtengwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakati Mohamed Muya amehamishiwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

Makatibu wakuu wengine waliohamishwa na Wizara zao mpya kwenye mabano ni Patrick Rutabanzibwa (Wizara ya Mambo ya Ndani) awali alikuwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dk Sergomena Tax (Wizara ya Afrika Mashariki) akitokea Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Wilson Mukama (Wizara ya Maji na Umwagiliaji) alikohamishiwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Blandina Nyoni (Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii) akitokea Wizara ya Maliasili na Utalii.

Naibu makatibu wakuu wapya walioteuliwa ni pamoja na Dk Philip Mpango aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Celestine Gesimba Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Seti Kamuhanda Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Mpango alikuwa Msaidizi wa Rais (uchumi) Ikulu, Seti Kamuhanda pia alikuwa msaidizi wa rais (hotuba) Ikulu na Gesimba alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Rais Kikwete pia amemhamisha Fanuel Mbonde aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi na kumpeleka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Makatibu wakuu waliostaafu kwa mujibu wa sheria ni pamoja na Vicent Mrisho aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bakari Mahiza, (Wizara ya Afrika Mashariki), Abel Mwaisumo (Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Charles Sanga a

No comments:

Post a Comment