Thursday, December 18, 2008
Mastaa watikisa kwa skendo
Wakati kalenda ikibakiza siku 13 (kuanzia kesho Ijumaa) kuuweka kando mwaka 2008 na kuingia mwaka mpya wa 2009, mastaa kibao nchini wametajwa kutikisa kwa skendo katika vipindi tofauti....
Waliowahi kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa kufanya madudu ni pamoja na Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim aliyekumbwa na skendo ya kuiba mume wa mtu aliyejulikana kwa jina la Mwinyi Ahmed na Miss Ilala namba 3, mwaka 2005 Jacqueline Patrick aliyedaiwa kumtapeli pedeshee mmoja maarufu shilingi milioni 5.
Wengine ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim ‘Nature’ kutoka Kundi la TMK Wanaume Halisi aliyedaiwa kumbaka ‘denti’ na kuburuzwa kwa ‘pilato,’ huku Khaleed Mohamed ‘TID’ akimaliza mwaka kwa kulala jela kwa miezi kadhaa kwa kosa la kujeruhi kabla ya kutolewa kwa msamaha wa Rais.
Ramadhani Msanja ‘Banza Stone’ kiongozi wa Bendi ya Bambino Sound na G Nako wa Kundi ‘mfu’ la muziki wa kizazi kipya la Nako 2 Nako walitia aibu kwa kunaswa na jeshi la polisi wakiwa na bangi.
Mwingine aliyechorwa alama mbaya mwaka huu ni Miss Tanzania namba 2, 2003 Mbiki Msumi ambaye alidaiwa kujihusisha na vitendo vya usagaji, ambaye hata hivyo aling’aka kutohusika na skendo hiyo.
Staa mwingine ambaye amekumbwa na skendo ni Msafiri Diouf rapa wa African Stars ‘Twanga Pepeta’ aliyedakwa na ‘njagu’ akihusishwa na tuhuma za uporaji simu kutoka kwa mwanamke mmoja huku Irene Uwoya naye akidaiwa kunaswa akivuta bangi hadharani.
Hata hivyo, licha ya mastaa hao na wengine ambao wamefunga mwaka kwa kuwa na skendo, mwaka huu watu maarufu wengi wamekuwa ‘wapole’ tofauti na mwaka jana ambapo kulikuwa na orodha ndefu ya mastaa waliofanya madudu ikiwemo kupiga picha za uchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment