KARIBU SANA

Friday, May 1, 2009

JUMBA LA KUUZA

FANI ya urembo nchini imeendelea kupakwa doa jeusi kwenye jamii, baada ya mpya tuliyoinasa hapa ‘juzi-kati’ kutufunulia uwepo wa jumba la kuwauza mamisi kwa watu wenye fedha ndefu a.k.a mapedeshee
Inanyetishwa kwamba kupitia jumba hilo, tayari mamisi kibao wamekwishapigwa bei, hivyo kutoa huduma ya ‘urojo’ kwa mapedeshee mbalimbali ambao wamekuwa na kawaida ya kuwapandia dau warembo wenye majina makubwa.
Kwa mujibu wa mbeya wetu wa kuaminika, jumba hilo lipo Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam na linamilikiwa na Miss Ruvuma 2005, Isabella Mpanda.

Mbeya wetu alitueleza kuwa Isabella alilizindua jumba hilo miaka miwili iliyopita na mara moja alianza kufanya biashara ya kuwauza warembo maarufu ambao wanamezewa mate na vidume mbalimbali nchini.

Alisema, muda mfupi baada ya kufungua biashara hiyo, alianza kupata msululu wa wateja ambao kila nukta ya mshale wa saa ilipokatika, walipiga simu kuweka ‘oda’ au kuulizia mali mpya.

“Uzuri yule dada ni mjanja sana, lakini ni nyoka! Anaweza kuingia sehemu yoyote, kwahiyo alitengeneza network (mtandao) ambao unamuweka karibu na watu wenye pesa wanaopenda kubadili ‘totoz’ kama nguo,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:

“Pamoja na kuunda mtandao wa uhakika kwa watu wenye nazo, hasa wale wanaopenda totoz, alijiweka karibu na kila mrembo mwenye jina kubwa, hasa wale wanaotokea mara kwa mara kwenye magazeti.”

Akiendelea zaidi, mbea huyo wa ukweli alisema, mara kwa mara mapedeshee mbalimbali humpigia simu Isabella, wakimtaka awaunganishe na warembo ambao wanakuwa wanawahitaji kwa kipindi husika.

Alisema, Isabella anapopewa kazi hiyo, hufanya juu chini na kumpata mrembo anayekuwa akihitajika kisha kumuunganisha na pedeshee husika kwa malipo ya kiasi kikubwa cha pesa.

Alisasambua kuwa kiasi cha pesa za malipo, hutegemeana na utoaji wa pedeshee mwenyewe na aina ya mrembo anayemtaka, kwani wapo wenye nazo lakini ni wagumu ‘kukata pochi’ la kutosha.

Alitaja kiasi cha pesa ambazo mara nyingi Isabella ‘hukatiwa’ na mapedeshee ili kuwaunganisha na warembo kuwa ni kati ya shilingi 300,000, 200,000 na 150,000.

“Chini ya hapo Isabella hawezi kukuunganisha. Yeye mwenyewe anaangalia hela ambazo atapata mgao, kwa mfano 150,000 hapo piga ua 50,000 ni yake,” alisema mbeya wetu.

Aliongeza kuwa katika mpango huo wa kuwaunganisha warembo na mapedeshee, mpaka sasa tayari Isabella ameweza kufanikisha baadhi ya mamisi kununua magari ya kutembelea kwa mapato wanayoingiza kupitia biashara ya kuuza miili yao.

Aidha, mbeya wetu aliwataja baadhi ya warembo waliowahi kupigwa bei na Isabella kuwa ni Miss Tanzania namba tano 2006-07, Irene Uwoya, mshiriki Miss Tanzania 2005-05, Maureen Gislary na muigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

Aliwaja wengine kuwa ni Miss Kanda ya Ziwa 2000, Rashida Wanjara, muigizaji Jacqueline Steven Mabango, mzazi mwenza wa Q-Chillah, Sheha Omar na Miss Ilala namba tatu 2008-09, Annette John.

Mbeya wetu, pia aliwataja baadhi ya warembo ‘wanaouza’ mitaa ya Uswahilini ambao hawavumi ‘kwa sana’ katika tasnia ya habari kama Angle Justas, Jamila msafiri, Rose John, Zuwena Mustafa na wengineo kuwa tayari ana vielelezo vyote kuwa wamewahi kupigwa bei na Isabella.

“Si hao tu, kuna warembo wengine kibao maarufu tayari wamekwishauzwa lakini siwezi kuwataja kwa sababu sina ushahidi, lakini hao nina uthibitisho ndiyo maana nimewataja,” alisema mtoa nyeti huyo na kuongeza:
“Baadhi ya mamisi wakiishiwa pesa, huwa wanampigia simu Isabella awatafutie mabuzi ili wapate ‘vijisenti’ vya kuwasukuma nayeye bila ajizi hutekeleza maombi yao.

“Kimsingi pale kwa Isabella ni kama danguro la mamisi au warembo maarufu, kwani baadhi yao hufika na kulala kabisa. Wengine wakiishiwa pesa wanahamia pale, wakitafutiwa mabwana na kuingiza kiasi cha pesa za kutosha ndiyo wanarudi makwao.”

Alisema: “Warembo ambao wamewahi kuhamia pale ni wengi, Irene Uwoya, Maureen, Annette, Jini Kabula, Jacqueline Steven Mabango na warembo wengine kibao ambao nimetaja orodha yao kuwa tayari wamekwishapigwa bei.”
Baada ya kuzinyaka ‘data’ hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi Kinondoni Mkwajuni na kujionea nyumba inayoelezwa kuwa ni jumba la kuwauza warembo wenye majina makubwa.

Kwa mujibu wa ushuhuda wetu, jumba linalotajwa si jumba bali ni chumba kimoja ambacho kina sifa zote za kuitwa geto.
Katika ushuhuda huo, mwandishi wetu aliwakuta warembo wengi wakiwa katika mapozi ya kihasara hasara juu ya kitanda chenye ukubwa wa futi sita kwa sita, huku wengine wakiwa wamejipumzisha kwenye ‘kapeti’ na kochi.
Akipangua hoja moja baada ya nyingine, Isabella alisema kuwa si kweli kwamba anajihusisha na biashara ya kuwauza warembo wenzake, bali watu wanamhisi hivyo.

“Nina marafiki wengi warembo, wengine ni wanafunzi wangu wa umisi ndiyo maana wanakuja kwangu kama marafiki, si kwa ajili ya kuwauza,” alisema Isabella na kuongeza:

“Hapa kwangu warembo wanakuja na kuondoka, hata mimi huwa nawatembelea na kulala kwao, hakuna kingine. Labda watu wanahisi kuwa nawauza kwa sababu wengine huwa wanafuatwa na ‘ma-boyfriend’ wao hapa hapa.
“Sasa watu wakiwaona wanaingia kwenye magari na wapenzi wao ndiyo wanavumisha kuwa tayari nimewauza wakati siyo kweli kabisa.”

Aidha, alipoulizwa ni kwanini anakiacha chumba chake kiwe kama geto, alijibu: “Chumba changu siyo geto, hawa ni marafiki zangu nipo nao, kama unaona hii ndiyo habari, kaandike unavyoweza.”

Gazeti hili, pia lilimtafuta Maureen na kumsomea tuhuma zake za kupigwa bei na Isabella ambapo alikanusha kuwahi kufanyishwa biashara ya mwili.

“Mimi nipo kwa Isabella muda mrefu, naishi kwake lakini hata siku moja sijawahi kununuliwa wala kuunganishiwa bwana, labda kama watu wanataka kuzusha yao. Isabella ni rafiki yangu wa kawaida tu, si wa kuniunganisha kwa wanaume,” alisema Maureen.

Kwa upande wake Sheha, yeye alijibu kuwa aliwahi kuishi kwa Isabella kwa sababu alimfuata rafiki yake Jacqueline Mabango ambaye alikuwa ‘anaminya’ kwenye geto hilo kabla ya kusafiri kwenda Iringa.

“Nilipotoka Iringa sikurudi tena kule kwa Isabella, nilifikia nyumbani kwetu Magomeni,” alisema Sheha a.k.a mama wa mtoto wa Q Chillah.

Naye Jini Kabula alijitetea kuwa Isabella ni rafiki yake kabla hajaingia Jumba la Dhahabu, kwahiyo huwa anakwenda kumtembelea na kulala kwake kama ‘mshkaji’ wake.

“Hajawahi kuniuza mimi, yule mtu ni rafiki yangu. Halafu mimi siyo malaya, kwahiyo siwezi kuuzwa kwa pesa,” alisema Kabula.

Jacqueline alisema kuwa aliishi kwa Isabella kwa muda, wakati alipokuwa akitafuta chumba. “Hajawahi kuniuza, kwani nilipopata chumba changu nilihama,” alisema.

Naye Jamila Msafiri alijitetea kuwa alilazimika kuishi kwa Isabella baada ya kukosa mahali pa kwenda. “Nilipata matatizo, nilipewa mimba na Mheshimiwa Temba (msanii Bongo Flava) akanitelekeza, kwahiyo nikakosa pa kwenda, nikaenda kujihifadhi pale kwa rafiki yangu,” alisema.

No comments:

Post a Comment