KARIBU SANA

Wednesday, April 1, 2009

Ushindi ya Kabula’ kuwekwa videoni

Msanii wa muziki wa Injili nchini, Kabula J. George, anatarajiwa kuirekodi albamu yake ya ‘Ushindi’ ambayo nyimbo zake zimeanza kuwashika watu wengi wanaozisikiliza kupitia vituo vya radio nchini, kwenye video
Akizungumza na safu hii, hivi karibuni, mwanadada huyo, alisema kuwa amechukua uamuzi huo ili kuwawezesha watu wengi zaidi kuupata ujumbe uliopo kwenye alibum hiyo kiurahisi ambao anaamini watamgeukia Mungu wao na kuachana na matendo maovu iwapo watamuona kabisa videoni.

“Naamini kupitia video nitaweza kuwashika wengi zaidi kwani pale kuna sauti na picha kwa pamoja naamini nitawabadilisha, tofauti na nyimbo za kidunia ambazo baadhi zimekuwa zikichochea watu kufanya maovu badala ya kumtumikia Mungu wao.”

Kabula alizitaja nyimbo hizo zitakazokuwepo kwenye albamu yake, ambazo amezinadi kuwa katika ubora wa hali ya juu ni: Ushindi, Tunaishi kwa Neema, Yesu wastahili, Yerusalem, Nikikumbuka, Dhihirisha, Hakuna muweza na Mshukuruni Mungu.

No comments:

Post a Comment