
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, leo aligeuka kioja baada ya kutinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, akiwa amenyuka suti kali na tai, lakini miguuni akiwa amevaa kiatu kimoja cheusi na mguu mwingine kandambili nyekundi, huku akitembelea mkongojo. Hali hiyo iliibua kimbembe Mahakamani hapo kiasi cha kuwafanya watu kusahau hata kufuatilia kesi kubwa ya ufisadi inayowakabili Yona, Mgonja na Mramba. Akionekana hana ‘time’ na mtu, Mtikila alitinga hadi katika chumba cha mawakili na kuwasalimia Yona, Mramba na Mgonja. Globalpublisherstz.com iliweza kumstopisha Mwanasiasa huyo mkongwe na kumuuliza kulikoni alikuwa 'ameripuka' kwa staili hiyo, ambapo alijibu kuwa Februari 16 akiwa nchini Zimbabwe, alivamiwa na joka kubwa aina ya 'Cobra' ambalo lilimg’ata mguu, lakini hakuweza kupata matibabu kwa siku tatu lakini alikuwa anakesha na kuomba.
Wakati mtandao huu ulipokuwa ukichonga na Mtikila, watu kibao wakiwemo mawakili, walikuwa wamemzunguka wakimshangaa ikiwa ni pamoja na kucheka, watu walizidi kuvunja mbavu baada ya mchungaji kusema kuwa alikaa siku tatu bila matibabu na alipona bila kutibiwa kwa sababu ya maombi tu. “Du! Mchungaji huyu kwa ‘Fix” hajambo, inawezekana vipi mtu ukapona baada ya kung’atwa na Cobra mwenye sumu kali bila matibabu? Labda aling’atwa na nge, maana Cobra ni saa chache tu mtu anavuta,” alisikika kijana mmoja akisema. Pichani Mtikila, (mwenye suti) akiwa na mpambe wake wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu.
No comments:
Post a Comment