
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kijana Ibrahimu Said ‘Ustaadhi’ aliyemzaba kibao Rais mstaafu wa awamu ya tatu Alhaji Aljasan Mwinyi ‘Ruksa’
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bi.Neema Chusi, baada ya mshatakiwa huyo kukili kosa jana. Chusi alisema kuwa amempa adhabu ya kutumikia mwaka mmoja jela kutokana na kutokuisumbua mahakama baada ya kukili kosa.
Alipotakiwa kujitetea, kijana huyo alitoa kihoja cha mwaka baada ya kuanza kuongea kiarabu ambapo alimuomba Hakimu kutafuta mkarmani wa Lugha hiyo.
Adhabu hiyo imeonekana kuwashangaza watanzania wengi ambao wanadai kuwa ni ndogo kulingana na kosa alilotenda kijana huyo la kumrabua kibao cha dharau Rais mstaafu wakati akihutubia Baraza la Masulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Hata hivyo wataalamu wa masuala ya sheria walioongea na mtandao huu wamedai kuwa alistahili adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria ambapo wamelinganisha kosa alilotenda kijana huyo na la mwandishi wa habari nchini Iraq la kumbonda aliyekuwa Rais wa Marekani George Bush ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu tu.
No comments:
Post a Comment