KARIBU SANA

Saturday, February 7, 2009

Ze Dudu 'Kama una beep we kenge tu'

Kwa kifupi naweza kusema sasa mzuka umempanda upya, kama ilivyokuwa jina la lebo yao (Mzuka Records) au kitambo kile wakati anatoka na ngoma kama Mwanangu huna nidhamu, Kunguru hafugiki, Nakupenda tu na nyingine ambazo zilimfanya aonekane ana njaa ya kuwa juu...
Mchizi anaitwa Godfrey Tumaini a.k.a Ze Dudu, Baba Willy na mwaka huu wa 2009 anajiita Mamba, ili kudhihirisha hilo hivi juzi tu ameachia pini mpya yenye jina hilo (Mamba) akiwa na wale mapcha waliyowahi kupiga shoo za kusisimua kwenye shindano la Bongo Star Search 2006 ambao wamekamata vesi ya pili.

ShowBiz ilipata bahati ya kuisikiliza ngoma hiyo ndani ya studio za Mzuka Records zilizopo Bahari Beach, Dar es Salaam kabla hata haijanza kwenda hewani na kugundua kwamba, mzuka wa 'Ze Dudu' hivi sasa umepanda zaidi kana kwamba ndiyo anataka kutoka.

Akisema na safu hii, mchizi alitamka kwamba, ngoma hiyo inamtambulisha yeye kama 'Mamba' na wale wote ambao hawajiwezi kwa mambo mengi anawaita Kenge. "Kama una 'beep' we ni kenge, kama huna hela ya bia we ni kenge, kama unapenda ofa we ni kenge, mimi ni Mamba kwasababu kila kitu najimudu,".

Aidha Dudu alisema kwamba, hiyo yote ni sanaa tu, kama kuna mtu atahisi hiyo ngoma imemlenga yeye ni juu yake. Kiukweli ni bonge moja la Hip Hop ambalo litamrudisha msanii huyo juu kama alivyokuwa zamani. Siku zote sisi ShowBiz huwa hatuongea sana, icheki ngoma yenyewe hapo kushoto.

No comments:

Post a Comment