
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti ndugu wa hili, Ijumaa Wikienda, jijini Dar es Salaam, Flora aliweka wazi kuwa, licha ya kuwepo kwa gonjwa hatari la ukimwi, lakini wamekuwa na uaminifu wa mapenzi na mtu wake wa karibu, ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake, hivyo kutumia zana hiyo muhimu.
“Mwanzoni tulipoanza mapenzi, tulikuwa tunatumia kinga, tumekuwa pamoja kwa muda mrefu, tunaaminiana katika tabia zetu, ndiyo maana tumesitisha kutumia kondomu,” alisema kwa aibu Flora.
Mnyange huyo ambaye amekuwa akikumbwa na kashfa kibao kila kunapokucha, aliongeza kuwa, kutokana na uamuzi huo wa kuwa na mpenzi mmoja tu, ndiyo maana hapendi kubadilisha wanaume mara kwa mara kwa kuogopa kunasa katika janga la UKIMWI linalopigwa vita na wanaharakati mbalimbali duniani.
Mrembo huyo alifafanua kuwa, kutokana na kumendewa mara kwa mara na wanaume wanaotaka penzi lake, yupo tayari kufanya kweli (kuolewa) ili kuepukana na midume yenye uroho wa ngono.
No comments:
Post a Comment