
Lisa alimwambia mwandishi wetu jana kwa njia ya simu kuwa habari zote zilizotapakaa mitaani ni za uongo na kusema kuna watu ambao wamepanga kumharibia sifa mbele ya jamii.
“Kuna watu wanatengeneza skendo, wanasema nimeachwa na mchumba wangu, mara nafanya mapenzi na Kanumba, yote hiyo ni kunivunjia heshima, mimi sijaachwa” alisema Lisa.
Kuhusu habari za kutengwa na kanisa lake la Sabato analoabudu kwa sasa alisema:
“mimi nasikia tu mitaani, wanasema sionekani kanisani Mwenge nilikokuwa nasali, kifupi kwa sasa nasali tawi la Mikocheni ambako ni karibu na nyumbani.”
No comments:
Post a Comment