
Amani ambalo lilitonywa juu ya mazingira magumu anayoishi msanii huyo, lilifanya uchunguzi ambapo juzi lilimfuma Diouf majira ya asubuhi akiwa amelala chini kwenye maboksi huku akiwa amejifunika kanga chafu.
Wakiongea na mwandishi wetu, baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao karibu na eneo hilo walidai kuwa, hayo ndiyo maisha anayoishi msanii huyo na kwamba, sasa hivi amekuwa kama chokoraa.
Walidai kuwa, Diouf amekuwa akilala katika eneo hilo chafu pamoja na mateja wenzake ambapo ifikapo jioni hutoka na kwenda kuomba pesa kwenye kumbi za burudani.
“Maisha ya Diouf yanasikitisha sana, huwezi kuamini kama ndiyo yulee aliyekuwa aking’ara kupitia bendi ya Twanga,” alisema mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Khalid huku akimtaka Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka kuangalia uwezekano wa kumsaidia kijana wake.
Amani baada ya kumkuta Diouf akiwa katika ‘gheto’ hilo lilifanya jitihada za kuzungumza naye lakini katika hali ya kushangaza, msanii huyo alichimba mkwara wa nguvu huku akimtaka mwandishi kuondoka katika aneo hilo kabla hajamfanyia kitu mbaya.
“Mimi sitaki kuongea na mtu yeyote… huko ni kuchoreshana tu, sitaki naomba uondoke sasa hivi kabla sijakufanyia kitu mbaya,” alisema Diouf huku akijifunika kanga.
Diouf kwa mara kadhaa amekuwa akiripotiwa na vyombo vya habari kupigwa chenga na maisha huku akidaiwa kuishi maisha ya kuombaomba hali inayomfanya akose heshima anayostahili katika jamii.
No comments:
Post a Comment