KARIBU SANA

Thursday, January 8, 2009

RAY C AFANYIWA KITU MBAYA UGANDA!


Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Ray C alipewa dili la kwenda kufanya makamuzi nchini humo na pedeshee huyo kwa makubaliano ya kulipwa dola za kimarekani 3,000, ambapo alifikia katika hoteli ya kifahari huku gharama zote zikiwa chini ya promota huyo.

Ilizidi kuelezwa kuwa, katika makubaliano yao Ray C alipewa kianzio cha dola za kimarekani 2,000 na akaahidiwa kumaliziwa kiasi kilichobaki baada ya shoo, huku gharama za malazi na chakula katika hoteli hiyo ya ‘kishua’ zikiwa chini ya pedeshee huyo.

“Makubaliano yao ya awali yalikuwa mazuri tu na Ray C aliona amepata dili la nguvu, lakini baada ya yule promota kuona amekamata mshiko mkubwa kwenye shoo aliyoiandaa, aliingiwa na tamaa ya pesa na kuingia mitini huku simu yake ikiwa ‘noti richabo’. Hakumlipa Ray C kiasi chake cha pesa kilichobaki na pia akaacha deni kubwa katika hoteli aliyokuwa analala msanii huyo,” alisema mtoa habari huyo.

Alizidi kuanika kuwa, mchezo mchafu aliochezewa Ray C na promota huyo ulimfanya ashindwe kuwa na uwezo wa kulipa deni alilokuwa akidaiwa hotelini hapo hali iliyomlazimu kuwasiliana na msanii wa nchini Uganda Jose Chamilione ambaye alikwenda kumuokoa katika aibu hiyo.

Ray C alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alikiri kufanyiwa kitu mbaya na promota huyo huku akimponda vilivyo kwa kusema kuwa, ni feki na haitatokea akaja kufanya naye kazi tena kama hatajirekebisha.

“Yule Promota ni feki na kwa kweli alinitia aibu. Yaani tumemuingizia pesa nyingi lakini tamaa ya pesa ikamuingia na akatutapeli. Ila niliweza kulitatua tatizo hilo kwa kushirikiana na Chamilione kwani pesa zangu nilikuwa nimeziacha Tanzania,” alisema Ray C.

No comments:

Post a Comment