
Wanaopinga wanadai Maximo ameshindwa kuweka programu inayoeleweka ya soka kwa miaka mitano ijayo, kushindwa kuiwezesha Tanzania kufuzu katika michuano iliyo mikubwa zaidi na kutoiweka soka ya Tanzania katika ramani inayoeleweka, wengi wanadai kazi hiyo heri apewe Kocha wa Vijana, Tinoco.
Wanaomtetea wanadai Maximo amefanikiwa kutokana na kuiwezesha Tanzania kwenda katika Mashindano ya CHAN, Ivory Coast pamoja na kuiweka Tanzania katika ramani ya soka kuliko huko nyuma.
Mtazamo wako ni upi? Je, Marcio Maximo anafaa au hafai?
Matokeo ya maoni hayo yatachapishwa pia katika gazeti la Championi Ijumaa
No comments:
Post a Comment