
Ay ambaye ni msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini aliwaambia waandishi wetu kuwa mama yake aitwaye Lydia Anania Yesaya alifariki kwa ugonjwa wa malaria na koo.
Alisema familia ilikuwa ikihangaikia matibabu yake kwa muda na kwamba mara ya mwisho alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyoko Dar es Salaam.
“Awali alikuwa na tatizo la ugonjwa wa koo, lakini baadaye akapata malaria ikabidi tumpeleke hospitali, madaktari walijitahidi kumtibu lakini hakupata nafuu” alisema AY kwa masikitiko.
Msiba wa mama wa msanii huyo uko eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo leo (Jumamosi) mamia ya watu maarufu wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatajia kushiriki mazishi.
Kampuni ya Global Publishers inampa pole AY na wanandugu wote kwa ujumla kwa msiba huo mzito, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.
No comments:
Post a Comment