KARIBU SANA

Thursday, March 3, 2011

Uchafu..MASTAA ‘tega nikutege’ katika Kiwanda cha Filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na shostito wake, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ wamebambwa wakinyonyana ndimi, Amani lina ushahidi mkononi.

Wawili hao walinaswa hivi karibuni maeneo ya Mango Garden, Kinondoni, Dar es salaam karibu na ofisi za ‘Jumba la Dhahabu’ wakiwa katika hali ya kimahaba huku wakijua kuwa, kitendo hicho hakiendani na utamaduni wa Mtanzania.

Katika pozi lao hilo, Kabula alionesha kumganda zaidi Jack huku mkono wake mmoja akiupeleka kwenye kiuno na vidole vya mkono wa pili vikiwa masikioni mwa mwenzake huyo.
“Khaa! Jamani mbona unapiga picha bila idhini yetu? Futa bwana, sisi tuko kwenye starehe zetu na ole wako tuzione gazetini,” aliropoka Jack baada ya kuona mwanga wa kamera ukiwamulika na kubaini kwamba, wamepigwa picha.

Wakati akija juu, hali ilikuwa tofauti kwa upande wa ‘mpenziwe’ Jini Kabula ambapo yeye alionekana kukifurahia kitendo hicho.

Mwandishi wetu hakuacha ‘gepu’ kukamilisha habari hii, alimfuata na kumuuliza kulikoni afanye kitendo hicho cha aibu:

“Wewe si umeshapiga picha, basi chukua ‘taimu’ yako, tuache na mambo yetu. Mimi naona ni kawaida kwani sisi hatuna hisia? Kama tumechoka na wanaume je!” Alikoroma Jini Kabula huku akimtazama mwandishi kuanzia chini hadi juu kama ishara ya kumdharau.

Baadhi ya watu waliokuwa katika eneo hilo na kushuhudia, walisikika wakilaani kitendo hicho huku wakisema kuwa ni uchafu mtupu. Walisema wasanii hao wamekithiri kwa vitendo viovu.

“Afadhali umewakuta ‘laivu’ maana huu ni uchafu. Tena hawa wamezoea, maana kila wakifanya maovu wanakanusha, tumewachoka. Na kama kioo cha jamii ndiyo hivi, hakuna maana,” alisema mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 45 hadi 50.
Baadhi ya wasanii wa ‘Jumba la Dhahabu’, walitoka nje na kukuta watu wamejazana wakiwashangaa wasanii wenzao kwa kitendo hicho.

Jack wa Chuz na Jini Kabula ni wasanii ambao hawakauki skendo chafu zinazomomonyoa maadili ya kitanzania zikiwemo za kuchangia wanaume na kuvaa nguo fupi za aibu kinyume kabisa na ‘taito’ yao.

No comments:

Post a Comment