KARIBU SANA

Thursday, April 2, 2009

KESI YA LIYUMBA KUFUTWA!


Kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Mipango wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Amatus Liyumba na mwenzake Deus Kweka, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imetakiwa kufutwa na Mawakili wao kwa mujibu wa kifungu cha sheria za nchi hii, kinachoutaka upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi ndani ya siku 60, vinginevyo kesi hiyo kufutwa. Kesi hiyo ina zaidi ya siku 60 na upelelezi bado haujakamilika. Pichani (kushoto) Liyumba akirudishwa Mahabusu leo mchana mara baada ya kesi yake kuahirishwa mpaka Aprili 13, mwaka huu, itakapotajwa tena kabla ya kusikilizwa Aprili 25, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment