KARIBU SANA

Monday, February 16, 2009

UWANJA MPYA WA TAIFA WAKABIDHIWA RASMI


Rais wa China Hu Jintao, amemkabidhi rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Uwanja mpya wa Taifa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania. Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika uwanjani hapo, Rais JK alimpongeza Rais wa awamu iliyopita, Benjamini Mkapa na kuzisifu juhudi zake kwa kusema yeye ndiye aliyekwenda kumuomba Rais huyo kujengewa uwanja huo mwaka 1998 akiwa madarakani. JK alisema yeye akiwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, ndiye aliyetia saini makubaliano hayo baada ya kuridhiana. Pichani kushoto Rais Hu JintaoChina akiupungia umati wa watu uliofurika uwanjani hapo.
Pichani moja ya vikundi vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo kikifanya vitu vyake.

Hawa ni baadhi ya watu waliofurika uwanjani hapo kushuhudia makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment