KARIBU SANA

Monday, February 9, 2009

MTASHA HUYU KIUNO CHAKE KAMA HAKINA MFUPA

Mtasha huyu pichani alitoa kali ya aina yake jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuonesha umahiri wa hali ya juu kwa kutikisa kiuno kama anacheza sindimba na kufanya umati wa watu kupiga vifijo ikiwa ni moja ya njia ya kumshangilia. Inshu katika Bonanza la Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa masauti’ lililofanyika Ufukwe wa Msasani Beach Club katika jiji la Dar es Salaam.



MZEE WA NYUMBA NYINGI YUKO NA ‘TOTOZ’
Pedeshee maarufu, Mzee wa nyumba nyingi usiku wa kuamkia leo alinaswa akiserebuka kwa madaha na ‘totoz’ katika onesho la Msondo Music Band lililofanyika ndani ya Africetre jijini Dar es Salaam.

KIUNO NACHO KUMBE DILI!

Kweli kiuno dili, baada ya kutoka kubangaiza kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini, mnenguaji wa TOT Respect Otilia Boniface, jana usiku alisema baada ya kujikusanyia mkwanja wa kutosha kwa kunengua sasa amerejea Dar kula ‘Bata’ raha kwa kwenda mbele. Mnenguaji huyo pichani akipagawishwa na rap za Greysoson Semsekwa aliye nyuma yake.

No comments:

Post a Comment