Liyumba ambaye alitoweka wiki moja iliyopita na kutolewa hati ya kusakwa kwake huku donge nono likitangazwa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwake, alitinga katika mahakama ya Kisutu majira ya saa 3 asubuhi akiwa kwenye gari aina ya Lite Ace lenye namba za usajili T 526 AVB akiwa na wakili wake Majura Magafu.
Baada ya kutua huku akilakiwa na umati mkubwa wa watu, Liyumba aliingia katika ofisi ya waendesha mashitaka ambapo baadaye alitolewqa akiwa chini ya ulinzi na kutupwa Selo kabla ya kupandishwa kizimbani akiwa sambamba na mtuhumiwa mwenzake Kweka.
Wakili wa upande wa mashtaka Prosper Mwangamila aliiomba mahakama kumfutia dhamana Liyumba kwa kuwa alikuka masharti na kwamba tayari hati ya kudakwa kwake ilikuwa imetolewa na imetekelezwa.
Hoja hiyo ilifafanuliwa zaidi na Hakimu anayeendesha kesi hiyo Bi.Khadija Msongo ambaye alidai kuwa Mahakama yake ndiyo iliyotoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba baada ya kubaini kuwa aliwasilisha mahakamani hapo Pasport iliyokwisha muda wake huku akiondoka na Passporti hai.
Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa vikali na wakili wa Liyumba Majura Magafu, ambaye alikili kuwa mteja wake aliwasilisha Passpoti hiyo kwa bahati mbaya.
Hoja hiyo ya Magafu, ilitupiliwa mbali na Mahakama, ambayo baadaye ilitangaza kumfutia dhamana Liyumba huku ikidai kuwa pamoja na kuidanganya mahakama kwa kuwasilisha Pasport iliyo 'Expire' lakini pia hati zake zote 10 za dhamana alizowasilisha mahakamani hapo zenye thamani ya Shiligi Milioni 800 ni batili
Hakimu Msongo alimtupa tena ndani Liyumba hadi Machi 10 ili aweze kutimiza masharti ya dhamana.
Hebu fuatilia matukio haya yafuatayo ujionee jinsi picha lilivyo kuwa mahakamani Kisutu leo.










No comments:
Post a Comment