
Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi akipakua chakula wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya UKIMWI duniani iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Zain, Dar es Salaam juzi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Zain Tanzania, Georgia Mutagahywa (kushoto) akiwaonyesha wafanyakazi wa kampuni hiyo jinsi ya kutumia kondomu za kike, wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mratibu kutoka Shirika la Kudhiti UKIMWI mahali pa kazi (ABCT), Frank Mwakyoma.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania, wakiinua mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani Dar es Salaam juzi
No comments:
Post a Comment