KARIBU SANA

Thursday, December 18, 2008

Filamu ya From China With Love

Filamu ambayo ni ya kwanza Tanzania kuchezwa katika kiwango cha kimataifa inayokwenda kwa jina From China With Love inatarajiwa kurushwa ‘Live’ katika kituo cha Televisheni cha Star TV...
Akiongea na gazeti hili, Meneja wa mradi wa Tollywood Movies, Abdalah Mrisho alisema kwamba, filamu hiyo itarushwa katika Kipindi cha Mcheza kwao siku ya Jumamosi saa 4:00 usiku na pia waandaaji wa filamu hiyo wataielezea kwa mara kwanza.
“ Filamu hiyo itaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumamosi ya Desemba 20, mwaka huu katika Televisheni ya Staa TV kwenye kipindi cha mcheza kwao, pia waandaaji wa filamu hiyo wataelezea utaalamu uliotumika katika kuikamilisha.

“Kwa wale ambao hawatabahatika kuiangilia filamu hiyo kwa siku hiyo ya Jumamosi kipindi hicho kitarudiwa tena siku ya Ijumaa saa 4:30 asubuhi,”alisema Mrisho.

Filamu ya From China With Love imetayarishwa na kampuni mama ya Tollywood Movies na ipo katika hatua za mwisho kabla ya kuingizwa rasmi sokoni Desemba 20, mwaka huu nchi nzima.

No comments:

Post a Comment